Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kapombe amefuata nyayo za Cantona, Ozil na Zidane

Fri, 8 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Beki Shomari Kapombe mwenye umri wa miaka 27 ametangaza kustaafu kuichezea timu ya Taifa Tanzania kutokana na majeraha yanayomuandama mara kwa mara.

Kapombe aliandika hayo katika ukurasa wake wa Instagram, huku maoni hayo yakiungwa mkono na baadhi ya wafuasi wake huku wengine wakimpinga.

Katika maelezo hayo, Kapombe aligusia kwamba majeraha yake yamemfanya kushindwa hata kushiriki katika klabu yake kwa asilimia mia, hivyo ameona ni muda sahihi wa kupunguza majukumu yake katika timu ya Taifa na kuwapa nafasi wengine.

Baada ya uamuzi huo wa Kapombe, Mwanaspoti limeangalia nyota wengine wa waliamua kustaafu kucheza timu za taifa kwa sababu mbalimbali wakiwa katika umri mdogo.

MARCO VAN BASTEN (31)

Mshambuliaji huyu aliyetamba akiwa na Ajax na AC Milan na timu ya taifa ya Uholanzi alilazimika kuacha kucheza soka akiwa katika kiwango cha juu kutokana na majeraha ya mara kwa mara ya kifundo cha mguu.

Pia Soma

Advertisement
Van Basten aliumia kifundo cha mguu akiwa na miaka 28, lakini alilazimisha kuendelea kucheza na alipofika umri wa miaka 31 aliamua kukaa pembeni baada ya maumivu kuzidi mguuni mwake.

Baada ya kuamua kustaafu aligeukia kuwa kocha na alijumuishwa katika benchi la timu ya Taifa ya Uholanzi akiwa kama kocha msaidizi.

ERICK CANTONA

Mshambuliaji wa Manchester United akiwa katika kiwango cha juu alitangaza kustaafu kucheza timu ya taifa ya Ufaransa kutokana na kukosa maelewano na kocha wa timu ya Taifa.

Cantona alijiondoa katika kikosi cha Ufaransa wakati ikijianda kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia 1998 na kuzua maswali mengi kwa uamuzi wake huo.

ZINEDINE ZIDANE

Kiungo bora zaidi kuwahi kutokea dunia alikuwa na uwezo mkubwa wa kutegeneza mashambulizi na kumiliki mpira.

Zidane aliamua kustaafu kucheza timu ya taifa ya Ufaransa baada ya Kombe la Dunia 2006 kufuatia kitendo chake cha kumpiga kichwa beki wa Italia, Marco Materazzi.

Baada ya tukio hilo Zidane aliamua kustaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 34.

JAMIE CARRAGER (29)

Alikuwa ni beki tegemeo katika kikosi cha Liverpool pale Uingereza, hilo lilitokana na namna ambavyo alikuwa akijituma kuhakikisha lango lao haliguswi guswi mara kwa mara.

Akiwa na Liverpool mwaka 2005 alishinda kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na klabu hiyo lakini mwaka 2007 aliamua kustaafu.

Carrager alistaafu kuichezea timu ya Taifa akiwa na umri wa miaka 29 tu.

Mesut Özil

Kiungo wa Arsenal, Mesut Özil aliamua kujiondoa kuchezea timu ya taifa ya Ujerumani baada ya kuzuka zogo kutokana na kitendo chake cha kupiga picha na rais wa Uturuki.

Kevin-Prince Boateng

Novemba 2011, Boateng alitangaza kustaafu kuichezea Ghana akiwa na umri wa miaka 24, hiyo ikiwa ni kutokana na kukataa kusafiri na timu iliyokuwa ikijianda na mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2012.

Chanzo: mwananchi.co.tz