Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kapombe Ashusha Presha Simba

KAPOMBE 1 Kapombe Ashusha Presha Simba

Sun, 3 Oct 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

BEKI mkongwe wa kulia wa Simba, Shomari Kapombe, ameshusha presha katika timu hiyo baada ya kupata nafuu ya majeraha yake ya kifundo cha mguu ‘enka’.

Kapombe alipata majeraha hayo katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United uliochezwa Mara. Katika mchezo huo, Kapombe alishindwa kumaliza dakika zote na kutolewa, huku nafasi yake ikichukuliwa na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Daktari Mkuu wa Simba, Yassin Gembe alisema beki huyo anaendelea vizuri baada ya kupata nafuu na huenda akawepo katika mchezo ujao dhidi ya Polisi Tanzania.

Gembe alisema kuwa beki huyo alipata majeraha madogo katika mchezo huo, lakini kwa hofu ya kupata maumivu zaidi wakampumzisha kwa makusudi.

“Kapombe amepata nafuu ya majeraha yake ya enka, ameanza mazoezi mepesi ya binafsi hivyo atakuwepo katika mchezo dhidi ya Polisi Tanzania.

“Kupona kwake kutaimarisha kikosi kutokana na umuhimu mkubwa wa Kapombe katika kikosi chetu,” alisema Gembe.

Chanzo: globalpublishers.co.tz