MTANGAZAJI wa Azam TV, Baraka Mpenja aliipa umaarufu Klabu ya Lipuli FC ya Iringa kutokana na jina la 'Kamwene' baada ya timu hiyo kupata matokeo mazuri mfululizo mbele ya Yanga msimu huu lakini leo Jumapili wamepokea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Mbeya City. Kabla ya Lipuli FC kuifunga Yanga bao 2-0, katika mechi ya nusu fainali kwenye Kombe la Shirikisho (FA), walikuwa wametoka kupoteza mchezo wa Ligi Kuu Bara ugenini dhidi Biashara United ya Musoma. Baada ya hapo wakaenda kufungwa tena na Ruvu Shooting kabla ya jioni ya leo Jumapili kukubali tena kichapo cha mabao 3-0, kutoka kwa Mbeya City mechi iliyochezwa Uwanja wa Samora, Iringa. Mabao matatu ya Mbeya City katika mchezo huo yalifungwa na Hamidu Mohammed dakika 63, Frank Ikobela dakika 81 na Peter Mapunda dakika 88. Mbali ya mchezo huo wa Ligi Kuu Bara kulikuwa na mechi nyingine kati ya Singida United waliokuwa nyumbani Uwanja wa Namfua walitoka sare 2-2 na JKT Tanzania. Mabao yote mawili ya Singiga United yalifungwa na mshambuliaji Habibu Kiyombo dakika 30 na dakika 50, wakati yale ya JKT Tanzania yakipachikwa na Dickson Cota katika dakika za nyongeza kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika na la pili lilifungwa na Samuel Kamuntu dakika 78. Mechi nyingine ilikuwa Coastal Union ambao walikuwa nyumbani Uwanja wa CCM Mkwakwani, Tanga walishinda bao 1-0, dhidi ya Mtibwa Sugar bao lililofungwa na Ayub Lyanga. Ushindi huo wa Coastal Union unakuwa kama umepoza machungu ya kupoteza mchezo wa mwisho waliofungwa na Simba mabao 8-1, katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Mechi nyingine ilikuwa kati ya African Lyon waliokuwa nyumbani walifungwa bao 1-0 dhidi ya Ndanda. Ikumbukwe kuwa hata kama African Lyon wangepata ushindi katika mchezo huu matokeo yasingeweza kubadilika kwa maana wameshashuka daraja msimu huu.