Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamusoko awashangaa Stars

64823 Kamusoko+pic

Sat, 29 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KIUNGO wa Yanga, Thabani Kamusoko amesema kikosi cha Taifa Stars kinapaswa kujilaumu chenyewe kwa kushindwa kupata ushindi mbele ya Kenya.

Kamusoko ambaye yupo hapa Cairo na timu ya Taifa ya Zimbabwe, alisema ameangalia mechi hiyo ya Kenya dhidi ya Tanzania na kwamba Stars kufungwa wamejitakia.

Kiungo huyo mkongwe alisema Stars baada ya kuongoza mara mbili hawakutaka kutulia na wakaendelea kucheza kwa papara.

Kamusoko aliongeza kuwa wakati Stars inaongoza walitakiwa kutuliza timu na kuwalazimisha Kenya kucheza mpira wanavyotaka wao.

Kiungo huyo alisema kitendo cha Stars kuendelea kushambulia kiliwapa nafasi Kenya kutafuta mabao ya kurudisha na kupata bao la ushindi.

Alisema Stars italazimika kujilaumu zaidi kwa kushindwa kutumia safu yao ya ushambuliaji ikiongozwa na Mbwana Samatta, Saimon Msuva na Farid Mussa ambao walikuwa bora na kama wangetulia hasa safu yao ya kiungo watatu hao wangepata mabao zaidi.

Pia Soma

“Nimeangalia ile mechi imeniuma sana niliona kama timu inafungwa halafu mimi nipo ndani ya uwanja,” alisema Kamusoko.

“Ile mechi Taifa Stars watajilaumu sana, ushapata kuongoza mara mbili kwanini usitulie ili uweze kumfanya mpinzani wako acheze unavyotaka wewe?” alisema Kamusoko.

Chanzo: mwananchi.co.tz