Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampeni uchaguzi Simba zashika kasi

24714 Pic+simba TanzaniaWeb

Wed, 31 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Zikiwa zimebaki siku sita kabla ya Klabu ya Simba kufanya uchaguzi wa viongozi, Novemba 4, kampeni zimeshika kasi kwa wagombea kujinadi kwa wanachama kuomba kura.

Simba ambayo imebadili mfumo wa uongozi baada ya kufanya mabadiliko ya Katiba na kuingia katika hisa, inatarajiwa kuchagua viongozi saba watakaoingia kwenye Bodi ya Wakurugenzi akiwemo Mwenyekiti na wajumbe sita wa Kamati ya Utendaji.

Wagombea 18 wanachuana vikali wakinadi sera zao kwa wapiga kura, lakini nafasi ya mwenyekiti haina presha kubwa kutokana na Swedi Mkwabi kukosa mpinzani baada ya mpinzani wake Mtemi Ramadhani kujitoa.

Mgombea wa nafasi ya ujumbe, Abdallah Migomba, alisema sifa za wajumbe ambao watateuliwa na mfadhili mkuu Mohammed Dewji 'MO' umemshawishi kuwania uongozi ili kuwakilisha wanachama kwenye bodi.

Naye Said Tully, aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, alisema anawania uongozi ili kuhakikisha anatimiza malengo manne.

Alitaja malengo hayo ni kuleta umoja na mshikamano, kulinda na kutetea masilahi ya wanachama, kulinda na kuendeleza mila na utamaduni wa Simba na kuendeleza mipango ya maendeleo ya Simba ndani na nje ya uwanja ikiwemo soka la vijana na wanawake.

Seleman Haroub alisema atashawishi wenzake ili kila mkoa kuwe na vituo vya vijana ambao baadaye wataunganishwa na wenzao wa Dar es Salaam.

Jasmine Badar alisema kipaumbele chake ni kulinda maslahi ya Simba na wanachama wake na ameahidi kutumia uzoefu wake kuunganisha matawi.

Chanzo: mwananchi.co.tz