Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kalaghe arudi upya Riadha Tanzania

Kallaghe.jpeg Kalaghe arudi upya Riadha Tanzania

Sun, 27 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

William Kalaghe amechaguliwa kuwa makamu wa rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) kwenye uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi hiyo na ile ya mjumbe mwakilishi wa kanda ya Pwani.

Kalaghe na Ikangaa walipata kura tisa kila mmoja huku Shaban Hiki akipata kura 6, matokeo yaliyopelekea wagombea hao wawili kupigiwa kura upya.

Kwenye awamu ya pili Kalaghe alipata kura 15 na Ikangaa 9.

Kalaghe aliwahi kuwa makamu wa rais kwenye uchaguzi uliopita kabla ya kuenguliwa kwenye usaili kwa kutokidhi vigezo kwenye uchaguzi mkuu uliofuatia mwaka jana.

Kwenye uchaguzi mdogo alirejeshwa katika usaili uliofanyika Novemba 23, na leo Novemba 27 amechaguliwa kwenye nafasi hiyo.

RT imefanya uchaguzi huo baada ya John Bayo aliyekuwa makamu wa rais na Robert Kalyahe kujiuzulu miezi kadhaa iliyopita.

Katika nafasi ya mjumbe mwakilishi wa kanda ya Pwani, Felix Chunga alipigiwa kuwa 21 za ndiyo na 3 za hapana.

Baada ya matokeo hayo, wajumbe wanaendelea na mkutano mkuu wa kawaida.

Chanzo: Mwanaspoti