Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaizer watamba kushambulia

KAIZER CHIEF 3?fit=1280%2C852&ssl=1 Kaizer watamba kushambulia

Sat, 22 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KOCHA Msaidizi wa Kaizer Chiefs, Dillon Sheppard amedai kwamba watatia chumvi kwenye kidonda cha Simba leo kwenye Uwanja wa Mkapa.

Amesisitiza kwamba hawajaja Tanzania kuzuia na kwamba hawatakubali kuona Simba ikitawala mchezo huo wa marudiano kwani wao watalinda ushindi wao na ikiwezekana kuongeza mabao.

“Mazoezi ya wiki hii yalikuwa vizuri na wachezaji wote wanajua ni nini tunapaswa kufanya uwanjani, tunapaswa kuhakikisha hawapati mabao mengi kuliko yale yetu ya mchezo wa kwanza,” alisema Sheppard ambaye viongozi wake walikuwa wakilalamikia muamuzi wa mechi ya leo kutoka Burundi kwa madai kuwa ataibeba Simba.

Alisema wanajua kwamba Simba itaingia na moto uwanjani wa kutaka kupata mabao ya mapema ili kuwavuruga lakini hawatakubaliana na hilo.

“Hatutaingia uwanjani kuzuia tu muda wote, lazima na sisi twende mbele tucheze mpira wetu. Lazima tuhakikishe hawadhibiti mchezo, maana wakifanikiwa tutakuwa kwenye hali mbaya na tunajua rekodi zao wakiwa kwao,” aliongeza.

“Tutapandisha timu ili wafunguke zaidi,” alisema kocha huyo akidai kwamba straika wake ghali, Samir Nurkovic amewaahidi mashabiki Sauzi kwamba lazima atupie tena leo.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz