Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kahata atua Dar es Salaam, asaini miaka miwili

65606 Kahataa+pic

Fri, 5 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kiungo mshambuliaji wa Gor Mahia, Francis Kahata ametua Dar es Salaam leo Alhamis Julai 04, 2019 na kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Simba .

Kahata aliyekuwa na kikosi cha Kenya ‘Harambee Stars’ katika fainali za Afcon aliwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere saa 9:15 alasiri ukiwa ni muda mfupi tu baada ya Taifa Stars kuwasili.

Kahata akiwa na wakala wake Agustino Ramadhani alipokelewa na Muhasibu wa Sumba, Selemani, ambaye aliwabeba katika gari yake aina ya Brevis na kuondoka nao.

Kahata atakutana na viongozi wa Simba kwa ajili ya kufanya mazungumzo wakiafikiana atasaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao na baada ya hapo ataondoka kwao Kenya.

Kahata alisema nimekuja Tanzania, lakini siwezi kuzungumza zaidi kwani sijapata muda kutokana nilikuwa katika kikosi cha timu ya Taifa katika mashindano ya Mataifa Afrika (Afcon), nchini Misri na baada ya kuwasili tu nyumbani niliunganisha ngege ya kuja huku.

"Muda ukifika kila kitu kitaweka wazi kwani nimekuja hapa Tanzania kwa ajili ya Simba na mazungumzo yetu yamekwenda vizuri kilichobaki ni kusaini mkataba wa kuitumikia timu hii na msimu ujao nitakuwa sehemu ya kikosi hiko," alisema Kahata.

Pia Soma

Kahata anamudu vyema kucheza kama mshambuliaji wa pili, winga wa pembeni pamoja na kiungo mshambuliaji namba nane, ana uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi za mabao, kupiga pasi za mwisho kwa washambuliaji na pia kuchezesha timu jambo ambalo litakuwa faida kwa Simba kutokana na ugumu wa mashindano na aina ya wapinzani ambao inaelekea kukutana nao kwenye Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye amekuwa akitumia zaidi mguu wake wa kushoto, anabebwa na sifa nyingine ambayo ni kuvunja ukuta wa timu pinzani pamoja na kufunga mabao na kutokana na kimo chake cha mita 1.78, Kahata ni mchezaji anayetumia zaidi akili pasipo kutegemea sana matumizi ya nguvu.

Pamoja na ubora wake akitegemewa kuziba nafasi ya Haruna Niyonzima ambaye hajaongezewa mkataba, Kahata anasajiliwa na Simba akiwa na uzoefu wa kutosha wa soka la Afrika ambapo amefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2018 akiwa na Gor Mahia ya Kenya na msimu wa 2018/2019 alikuwemo kwenye kikosi cha timu hiyo kilichofuzu hatua ya robo fainali ya mashindano hayo, huku pia akiwa ametwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Kenya mara tatu mfululizo.

Ameshakutana mara kadhaa na timu za Tanzania katika mashindano mbalimbali ambapo mwaka 2018, alikumbana na Yanga mara mbili kwenye Kombe la Shirikisho na mwaka huu alikutana na Mbao FC kwenye Kombe la SportPesa.

Pamoja na mambo hayo mawili, sababu nyingine ambayo huenda ikawa imeishawishi Simba kumsajili Kahata, ni gharama nafuu za dau lake kwani kwa sasa mkataba wa kiungo huyo na Gor Mahia umemalizika hivyo anajiunga kama mchezaji huru ikimaanisha kuwa Simba haitaingia gharama mara mbili ambazo ni ile ya kuvunja mkataba na fungu la mchezaji kwa ajili ya kutia saini.

Chanzo: mwananchi.co.tz