Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kahata amtumia salamu Shikalo

68206 Kahata+pic

Thu, 25 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

ROSTENBURG. Mchezaji wa Simba, Francis Kahata, ametuma salamu kwa kipa mpya wa Yanga Farouk Shikalo.

Kahata aliyesajiliwa na Simba akitokea Gor Mahia ya Kenya alidai licha ya ubora wa Shikalo, lakini anafungika.

Shikalo anayepewa nafasi ya kuwa kipa namba moja Yanga amejiunga na klabu hiyo akitokea Bandari ya Kenya.

Kahata alisema Shikalo anaweza kufungwa katika mchezo wao na Simba unaotarajiwa kufanyika Januari 4, mwakani.

“Shikalo ni kipa mzuri lakini anafungika namjua kwa sababu tulikuwa naye katika mashindano ya Ligi Kuu na timu ya Taifa,” alisema Kahata.

Mchezaji huyo alisema kazi ya mshambuliaji ni kufunga mabao, hivyo atapambana kuipa Simba mafanikio katika mashindano ya msimu ujao.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz