Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagere noma! ainyanyua Simba kwa Mkapa

Kagere Full Pic Data Kagere noma! ainyanyua Simba kwa Mkapa

Thu, 4 Nov 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Simba imevuna lama nyingine tatu kwenye Uwanja wa Mkapa baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Namungo kwa bao liliwekwa wavuni na Meddie Kagere.

Kagere aliyeingia dakika za nyongeza alimalizia kwa kichwa krosi ya Mohammed Hussein 'Tshabalala' na kumshinda mlinda mlango wa Namungo Jonathan Nahimana.

Katika mchezo huo Namungo, Simba walionekana kuendelea kusumbuliwa na kasumba ya kutumia nafasi ambazo wamekuwa wakitengeneza ikiwemo moja ya wazi aliyopoteza Kibu Denis.

Aliyekuwa akiongoza mashambulizi kwa wekundu hao wa msimbazi alikuwa ni mfungaji bora wa msimu uliopita, John Bocco kabla ya baadae kuingia Meddie Kagere.

Kagere ndiye aliyewapa raha mashabiki wa Simba mwishoni kabisa mwa kipindi cha pili, Mrwanda huyo alipachika bao lake la pili msimu huu na kuwanusuru mabingwa hao watetezi kuvutwa Shati na Namungo ambao walikuwa pungufu.

Namungo iliwabidi wamalize pungufu baada ya kiungo wao,  Abdulziz Makame kuonyeshwa kadi nyekundu kufuatia kumchezea vibaya, Shomari Kapombe dakika ya 54.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz