Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagere aiongezea kasi Simba ikishinda mabao 2-1

52800 Pic+simba

Wed, 17 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tanga. Timu ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union mchezo uliofanyika leo Jumatano kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Mabao ya Simba yaliwekwa wavuni na Meddie Kagere dakika ya 48 na msumali wa mwisho aliuweka wavuni kwa mkwaju wa penalti dakika ya 68.

 Bao la mapema kwa Coastal Union lilifungwa na Raizin Hafidh dakika ya kwanza.

Kocha wa Simba, Patrick Aussems amelalamikia sehemu ya kati ya uwanja wa Mkwakwani akisema kwamba, ni mbaya kwa kuwa ni kipara. Hivyo ilikuwa ikiwaumiza wachezaji wake lakini baada ya mapumziko waliuzoea na kupata mabao mawili.

Kocha wa Coastal Union, Mgunda amesema wamecheza na timu yenye wachezaji walio na uzoefu mkubwa waliotumia makosa yaliyofanywa na Coastal Union.

Hata hivyo amesema ligi hii imefikia mahala pagumu kwa kuwa kila timu inapigania nafasi na kwamba itaendelea kuwa ngumu

Related Content

Kikosi cha Simba kilichoanza  kilikuwa ni: Aishi Manula,Nicholas Gyan, Asante Kwasi, Yusufu Mlipii, Erasto Nyoni, Said Ndemla, Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga, Meddie Kagere, Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima.

Wengine ambao waliaanzia benchi ni Deogratisa Munish, Mohamed Hussen, Paul Bukaba, Mohamed Ibrahim, Adam Salamba, Cleotus Chama na Rashid Juma.



Chanzo: mwananchi.co.tz