Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagere achimbwa mkwara mzito

15962 KAGELE+PIC TanzaniaWeb

Thu, 6 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere, anaongoza kwa kufunga mabao katika Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini Pastory Athanas ametamka kuwa atakula naye sahani moja.

Athanas anayecheza katika kikosi cha Mbao FC, amesema ana imani atampiku Kagere katika mbio za kutwaa tuzo ya mfungaji bora katika mashindano hayo.

Kauli ya Athanas ni majibu kwa Kagere ambaye ameahidi kuipa Simba ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya pili mfululizo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Rwanda mwenye asili ya Uganda, anaongoza kwa kufunga mabao matatu katika ligi hiyo iliyofikia raundi ya tatu.

Athanas alisema licha ya kufunga bao moja katika mashindano hayo, ana uhakika ataongeza mengine katika ligi hiyo inayoshirikisha timu 20.

 “Ligi ndio imeanza Kagere amefunga mabao matatu nitapambana naye kuhakikisha kila mechi ninayocheza nafunga, msimu huu nataka kuibuka mfungaji bora,”alisema Athanas.

Chanzo: mwananchi.co.tz