Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagere aanzia kwa APR

10563 Pic+kagere TanzaniaWeb

Tue, 3 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mshambuliaji mpya Meddie Kagere ataiongoza safu ya ushambuliaji ya Simba leo dhidi ya APR ya Rwanda, saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mshambualiaji huyo wa zamani wa Gor Mahia ya Kenya atakuwa akisawaidiwa na Adam Salamba na Marcel Kaheza katika kuhakikisha Simba inapata ushindi katika mchezo huo.

Kagere ndiye atakuwa anatazamwa zaidi katika mechi hiyo, kwani mashabiki wake watahitaji kuona anafanya nini baada ya Kaheza na Salamba kucheza mechi ya ufunguzi dhidi ya Dakadaha walioifunga mabao 4-0.

Kagere atakuwa na kibarua kigumu kuonyesha uwezo ambao unasubiriwa na mashabiki hasa kutaka kuona atawafanyia nini katika ligi ijayo na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kikosi ch Simba

Kipa Ally Salim, Ally Shomari, Mohammed Hussein, Paul Bukaba, Pascal Wawa, Mzamiru Yassin, Said Ndemla, Mwinyi Kazimoto, Meddie Kagere, Adam Salamba, Marcel Kaheza.

Akiba:

Deogratius Munishi, Jamal Mwambereko, James Kotei, Nicholaus Gyan, Rashid Juma, Abdul Hamisi, Mohammed Rashid.

Chanzo: mwananchi.co.tz