Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagere, Salamba tishio jipya Kagame

10570 Pic+simba TanzaniaWeb

Tue, 3 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Washambuliaji Meddie Kagere na Adam Salamba wamefanya kile kilichosubiliwa na mashabiki baada ya kuiongoza Simba kuichapa APR ya Rwanda kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mkongwe Kagere aliwainua mashabiki wa Simba dakika 91, kwa kufunga bao lake la kwanza akiwa na timu hiyo kwa mkwaju wa penalti iliyotokana na Mnyarwanda huyo kuangushwa kwenye eneo la hatari na beki wa APR.

Wakati Kagere akifungua kitabu chake cha mabao, chipukizi Salamba alifunga bao la tatu katika mashindano ya Kombe la Kagame akiunganisha shuti la Marcel Kaheza na kuisawazishia Simba dakika 76, wakati mabingwa wa Rwanda, APR ilipata bao lake la kuongoza lililofungwa na Nkinzingabo Fiston.

Ushindi huo unaifanya Simba kuongoza Kundi C kwa tofauti ya mabao baada ya kufunga kwa pointi sita sawa na Singida United na kujihakikisha kufuzu kwa robo fainali.

Simba ikicheza mbele ya mashabiki wake wachache kwenye Uwanja wa Taifa, kocha Masoud Djuma aliamua kuanzisha mshambuliaji Kagere aliyesajili kutoka Gor Mahia ya Kenya pamoja na Salamba na Kaheza.

Salamba alipata nafasi mbali ambayo ya kwanza ilikuwa krosi kutoka kwa Ally Shomary na alibinuka tikitaka ambayo haukulenga lango na alitoka nje.

Nafasi nyingine ambayo Salamba alipata ilikuwa pasi ya uchonganishi ambayo alishindwa kuiwahi na kipa wa APR Ntaribi Steven kuokoa hatari hiyo.

Simba waliendelea kufanya mashambulizi ya hapa na pale ndani ya dakika zote 45 za kipindi cha kwanza lakini hawakuweza kupata bao.

APR ambao walipoteza mechi ya kwanza dhidi ya Singida United kwa kufungwa bao 1-0 walionekana kujipanga katika mechi na Simba kwa kuwazuia kipindi cha kwanza kwa kutofanya makosa katika nafasi yao ya ulinzi.

Katika kipindi cha kwanza APR walitengeneza nafasi moja ambayo lilipigwa shuti nje ya boksi na Emmanuel. Imanishimwe ambalo lilipanguliwa na kipa wa Simba Ally Salim na kuwa kona.

Chanzo: mwananchi.co.tz