Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagere, Nonga vitani Ligi Kuu

89881 Kagere+pic Kagere, Nonga vitani Ligi Kuu

Fri, 27 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati Simba na Lipuli zikiteremka uwanjani leo kuwania pointi tatu, vita kubwa ipo kwa washambuliaji Meddie Kagere na Paul Nonga.

Simba na Lipuli ya Iringa zitavaana katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kivutio katika mchezo wa leo ni vuta ya ufungaji mabao baina ya Kagere (Simba) na Nonga ambao wamekuwa na viwango bora msimu huu.

Kagere anaongoza kwa ufungaji akiwa na mabao manane na Nonga saba, hivyo kila mmoja atakuwa na shauku ya kufunga ili kuboresha akaunti yake.

Pia mchezo huo utawakutanisha washambuliaji wawili Miraji Athumani wa Simba na Daruwesh Saliboko ambao kila mmoja amefunga mabao sita. Miraji amekuwa na kiwango bora na ndiye aliyefunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting kabla ya ligi kusimama kupisha mechi za timu ya taifa.

Saliboko ndiye mkombozi wa Lipuli kwani amekuwa akifunga mfululizo na ameingia katika orodha ya wachezaji watatu waliofunga ‘hat trick’ msimu huu akiungana na Ditram Nchimbi na Obrey Chirwa. Timu hizo zimekuwa na upinzani mkubwa kutokana ubora wa vikosi vyao huku rekodi baina yao ikizidi kuongeza ushindani wa mchezo wa leo.

Lipuli imefungwa mara moja kati ya mechi nne ilizocheza dhidi ya Simba tangu ilipopanda Ligi Kuu. Februari 26 ilishinda mabao 3-1 na mechi zilizobaki zilitoka sare ya bao 1-1 mara mbili na mechi moja suluhu. Katika ushindi wa 3-1, mabao ya Simba yalifungwa na Clatous Chama (mawili) na Kagere na lile la Lipuli lilifungwa na Nonga. Kocha Sven Vandenbroeck anaiongoza Simba mara ya kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara tangu alipopewa mikoba ya Patrick Aussems. Juzi aliiongoza timu hiyo kupata ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya AFC Arusha katika mechi ya Kombe la FA.

Chanzo: mwananchi.co.tz