Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagere, Chama hawaendi kokote-Dewji

50664 Pic+moo

Fri, 5 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya Simba, Mfanyabiashara Mohammed Dewji ametamba kuwa klabu hiyo haiko tayari kuwaachia nyota wake tegemeo kikosini hasa Meddie Kagere na Clatous Chama hata kama ofa nono za timu nyingine zitakuja mezani.

Akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Dewji alisema kuwa Simba inataka kushindana kimataifa hivyo kupoteza wachezaji wazuri ni hasara kwao.

"Sisi tunajenga timu ili iweze kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa sasa hauwezi kujenga timu huku unawaachia wachezaji wako muhimu kama Kagere na Chama. Na ukiangalia utaona tunawapa huduma nzuri na mfano bonasi tunayowapa ni zaidi ya Shilingi 1 bilioni. Nadhani hapo utaona ni kwa jinsi gani tunajipanga kuhakikisha tunakuwa na timu bora.

 Kagere na Chama wana mikataba ambayo bado haijaisha hivyo tutaendelea kuwa nao na nafahamu kuna wachezaji wengine nane ambao mikataba yao inaisha. Wale ambao kocha ataonyesha kuwahitaji watabaki na kwa bahati mbaya wengine hatutoendelea nao," alisema Dewji.

 Dewji alisema baada ya mafanikio waliyoyapata msimu huu, mkakati wa bodi ya klabu hiyo ni kuifanya Simba iweze kufanya vyema zaidi kimataifa



Chanzo: mwananchi.co.tz