Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagera sugar yaendeleza ubabe kwa Simba

56706 Pic+matokeo+simba

Fri, 10 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Simba imelala kwa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaa.

Kagera walipata bao hilo la ushindi dakika ya 41, wakati Mohammed HKagera ussein 'Tshabalala' akijaribu kuokoa.

Tulio hilo ni kutokana na mpira wa krosi uliopigwa ndefu lakini wakati Tshabalala anakwenda kuokoa Kipa Aishi Manula naye alikwenda wakajikuta wanagongana na kuuruhusu mpira kuingia golini kwao.

Bao lililoleta hali ya kutoelewala wachezaji hao na Manula kumkoromea Tshabalala ambaye ilimbidi ahame eneo hilo na kwenda katikati ya uwanja.

Hata hivyo,  kabla ya mpira huo kumalizika katika mabadiliko yaliyofanywa na Kocha Patrick Ausems kumtoa James Kotei na kumuingiza Jonas Mkude kumewatoa povu mashabiki wa Simba.

Mashabiki hao ambao awali walikuwa walitatamani Mkude aingie huku wakipaza sauti wakitaka kiungo huyo aingie walionekana kukasirishwa baada ya kocha kumtoa Kotei.

Habari zinazohusiana na hii

Huku wakipaza sauti kulalamikia sumabadiliko  hiyo, mashabiki walidai kocha hakupaswa kumtoa Kotei sababu alikuwa fiti.

"Bora angemtoa Mzamiru Yassin, sio kotei," walisikika baadhi ya mashabiki huku wengine wakiwapinga na kudai soka la Kagera Sugar linahitaji wachezaji wenye nguvu kama Mzamiru.

"Kocha kuna kitu amekiona, Kagera wanatumia nguvu na akili, Mzamiru pia anatumia nguvu huwezi kumtoa," alisikika Shabiki aliyejitambulisha kwa Jina la Ramadhan akiwakosoa wenzake.

Mbali na mabadiliko hayo, kocha pia aliwatoa Mohamed Ibrahim na Hassan Dilunga na kuwaingiza Clatous Chama na Rashid Juma.



Chanzo: mwananchi.co.tz