Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagera Sugar yatangaza vita Kaitaba

Baraza Kagera ED Kagera Sugar yatangaza vita Kaitaba

Thu, 13 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Baraza alisema lengo lake ni kuona kikosi hicho kinavuna pointi zote tisa kwenye uwanja wa nyumbani wa Kaitaba na kujiondoa kwenye hatari ya kushuka daraja.

Kocha huyo huo ni ushindi wa kwanza tangu alipochukuwa majukumu ya kukinoa kikosi cha timu hiyo na bado wanapambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye michezo iliyobakia.

Alizitaja mechi zilizobakia watakazocheza nyumbani ni dhidi ya Ruvu Shooting itakayofanyika Mei 17, mwaka huu halafu wataikaribisha Ihefu SC na baadaye Tanzania Prisons.

"Tumejipanga kuhakikisha tunapata pointi tatu katika kila mechi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuendelea kucheza ligi kwa msimu ujao. Ligi imekuwa na ushindani mkubwa sana na kila mmoja anahitaji kupata pointi tatu, kwa sababu kuna watu wanahitaji ubingwa na wengine kujinasua kushuka daraja kama ilivyo kwetu.”

“Tuko katika hali mbaya nina imani kwa kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wangu katika mchezo wetu dhidi ya Mwadui, tena ugenini, dalili za kubakiza pointi tisa nyumbani zitatimia,” alisema Baraza.

Kagera Sugar yenye pointi 30 iko katika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kucheza michezo 29 wakati vinara wa ligi hiyo ni mabingwa watetezi, Simba yenye pointi 61.

Chanzo: ippmedia.com