Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagera Sugar yaiweka mtegoni Simba

85414 Pic+kagera Kagera Sugar yaiweka mtegoni Simba

Sat, 23 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

SIMBA ndio Baba Lao. Hivyo ndivyo unaweza ukasema mara baada ya kuongoza ligi kwa siku 70 tangu ligi ilipoanza Agosti 24 mwaka huu, huku Kagera Sugar ikiwa katika nafasi ya kutaka kupindua meza leo Ijumaa endapo itapata matokeo kwenye mchezo wake dhidi ya Lipuli. Simba ipo kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 22 baada ya kucheza michezo tisa wakati Kagera Sugar ambayo inatarajia kuwa mwenyeji wa Lipuli ina pointi 20 endapo itapata matokeo basi itafanikiwa kumshusha Simba. Kagera Sugar imecheza michezo 10 na kufanikiwa kufikisha pointi hizo ambazo imewazidi pointi mbili wapinzani wao Lipuli wenye pointi 18 kwenye michezo 10 waliyocheza. Mbali na mchezo huo wa Simba leo kuna michezo mingine saba ambayo inatarajia kuchezwa katika viwanja mbalimbali ambapo macho ya mashabiki wengi yatakuwa Uhuru kwenye mechi  ya Yanga na JKT Tanzania, Kagera na Lipuli ambao utatoa taswira ya Simba kuendelea kubaki kuongoza ligi au kushushwa. Endapo Karera watapata matokeo basi watamshusha Simba kileleni baada ya kukaa hapo kwa muda mrefu na kushindwa kushushwa kutokana na timu hiyo kufanya vizuri. Simba wao watakuwa wageni wa Ruvu Shooting  kesho Jumamosi na endapo watapata matokeo mazuri basi watarudi nafasi yao, michezo mingine inayochezwa leo ni Biashara na Mtibwa Sugar, Tanzania Prisons na Mwadui, Namungo na Coastal Union, Ndanda, Polisi Tanzania na Alliance na KMC.

Chanzo: mwananchi.co.tz