Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaduguda apewa mikoba ya Mkwabi, Try Again arudi Simba SC

85114 Pic+kaduguda Kaduguda apewa mikoba ya Mkwabi, Try Again arudi Simba SC

Fri, 22 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba, imemteua Mwina Kaduguda kuwa kaimu mwenyekiti wa klabu hiyo.

Kaduguda anakaimu nafasi hiyo baada ya mwenyekiti aliyechaguliwa na wanachama, Swedy Mkwabi kujihudhuru nafasi yake hivi karibuni.

Mkwabi alijiuzulu nafasi ya mwenyekiti ikidaiwa kushindwa kuelewana na baadhi ya viongozi wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo kwenye kwa vyombo vya habari ilisema Kaduguda ambaye ni mjumbe wa bodi ya klabu hiyo atakaimu nafasi ya mwenyekiti ikiwa ni uteuzi uliofanywa na Bodi chini ya ibara ya 50 ya katiba Simba ya mwaka 2018.

Taarifa hiyo pia ilisema Bodi ya Wakurugenzi imemteua Salim Abdallah ‘Try Again’ kuwa makamu mwenyekiti wa Bodi hiyo.

Taarifa hiyo ilisema tarehe ya uchaguzi wa kujaza nafasi ya mwenyekiti itatangazwa hapo baadaye na bodi ya Wakurungezi.

Kaduguda aliwahi kuwa katibu mkuu wa Simba wakati timu hiyo ikiwa chini ya mwenyekiti Hassan Dalali.

Pia, Abdallah ‘Try Again’ ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa muda wa Simba wakati aliyekuwa mwenyekiti Evans Aveva na makamu wake Godfrey Nyange ‘Kaburu’ walipokuwa gerezeni.

Try Again ndiye aliyesimamia mchakato wa mabadiliko ya Simba pamoja na uchaguzi wa Simba uliomwingiza madarakani Mkwabi.

Chanzo: mwananchi.co.tz