Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KUELEKEA KILELE CHA SIKU YA MWANACHI YANGA YAMTAJA MGENI RASMINI

Kikwete 1?fit=800%2C445 KUELEKEA KILELE CHA SIKU YA MWANACHI YANGA YAMTAJA MGENI RASMINI

Thu, 27 Aug 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Aliyekuwa Rais wa Awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ndiye atakayekuwa Mgeni Rasmi wa siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi Agosti 30 .

Kilele hicho cha siku ya Wananchi kitafanyika katika Uwanja wa Mkapa na klabu ya Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Eaglenor ya Burundi.

Yanga Jana ilitarifu kuwa kocha Cedric Kaze aliekua anatarajiwa alitarajiwa kuwasili nchini kesho Ijumaa na mabingwa hao wa kihistoria Tanzania ametoa udhuru kutokana na matatizo yake ya kifamilia.

Taarifa imeeleza kocha huyo ameomba wiki tatu zaidi kutokana na matatizo hayo , hivyo uongozi wa Yanga umeona ni vyema kutafuta kocha mwengine kutoka katika orodha ya waliopeleka maombi awali haraka iwezekanavyo.

Habari zinaeleza kuwa miongoni mwa makocha ambao wanatajwa kuingia kwenye hesabu za Yanga ni pamoja na aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omong pamoja Kocha Mkuu wa Taifa Stras, Ettiene Ndayiragije.

Kwa habari za michezo tembelea www.dimbani.co.tz

Chanzo: zanzibar24.co.tz