Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMC yaitandika Sharks

70213 Kmc+pic

Wed, 7 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KIKOSI cha KMC, leo Jumanne asubuhi wamecheza mechi ya kirafiki na kushinda mabao 2-1, mechi hiyo ilichezwa uwanja wa Uhuru dhidi ya Kariobang Sharks ya Kenya

Kariobang juzi Jumapili walitoka sare 1-1 na Yanga katika kilele cha Wiki ya Mwananchi uwanja wa Taifa.

Mabao ya KMC, yalifungwa na wachezaji wapya Nogues Serge na Vitalis Mayanga aliyesajiliwa akitokea Ndanda.

Mayanga alisema mchezo huo ulikuwa muhimu kwao kwa majaribio kwani wanakwenda kucheza mechi ya Kimataifa na AS Kigali ya Rwanda ambayo inaendana kabisa na uwezo wa timu ya Sharks ambao wamecheza nao.

"Mwanzo mzuri kwangu kufunga katika mchezo huu lakini hata kwa timu kwa ujumla kupata ushindi kwani nina imani benchi la ufundi kuna kitu wamekiona kutoka kwetu kabla ya mechi ya ushindani,"

"Kikubwa tunaendelea na maandalizi ambayo kwetu kama wachezaji ni mazuri na tunapata kila kitu kuelekea mwanzo wa msimu mpya," amesema Mayanga.

Chanzo: mwananchi.co.tz