Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMC FC yatamba kurudisha maumivu Mtibwa Sugar

KMC FC KMC FC yatamba kurudisha maumivu Mtibwa Sugar

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha KMC FC kesho Jumamosi (Desemba 18) kitashuka katika uwanja wa Manungu Turiani Mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa saaa 10:00 Jioni.

Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni ambayo iliwasili mkoani hapa jana ikitokea Jijini Dar es Salaam imefanya maandalizi yake ya mwisho kabla ya mchezo wa kesho na kwamba kikosi hicho cha wana Kino Boys kikotayari kwa mtanange huo muhimu.

KMC FC ambao watakuwa ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar inahitaji kufanya vizuri katika mchezo huo ili kuendelea kujiimarisha zaidi katika msimamo wa Ligi kuu ya NBC licha ya kuwa inakwenda kukutana na Timu yenye ushindani lakini KMC ni bora zaidi na kwamba maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa.

KMC FC ambayo ipo nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania bara imejiandaa vema kupata matokeo mazuri ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha kuwa kama Timu inapata ushindi kwenye michezo yake yote licha ya kuwepo kwa ushindani mkubwa kwa Timu nyingine zinazoshiriki Ligi Kuu.

“Ukiangalia kwenye msimamo wa Ligi bado kunaushindani mkubwa, kila Timu inahitaji kupata matokeo mazuri, lakini KMC tunahitaji ushindi mzuri kwa umuhimu wa namna yake, mchezo wa kesho tunafahamu kuwa utakuwa mgumu lakini sisi tunakwenda uwanjani kupambania alama tatu muhimu.

Ukiangalia wapinzani wetu kwenye michezo yao wamefanya vizuri, lakini haifanyi sisi tukakosa matokeo, kwa sababu kila mmoja amejipanga kwa namna yake, kikubwa tunamuomba mwenyezi Mungu atuamshe salama ili vijana wetu wakaipambanie Timu na kupata matokeo ambayo tunayahitaji kwa maana ya alama tatu.

Imetolewa leo Disemba 17

Na Christina Mwagala

Ofisa Habari na Mawasiliano KMC FC- Morogoro

Chanzo: www.tanzaniaweb.live