Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KARIAKOODABI: Kagere, Makambo wapewa mikoba ya Okwi, Ajib

19514 Pic+kagere TanzaniaWeb

Thu, 27 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Maisha yanakwenda kasi katika soka la Tanzania hasa katika klabu za Simba na Yanga zilipokutana mara ya mwisho Aprili 29, 2018, nyota waliokuwa kivutio ni Emmanuel Okwi kwa Simba na Ibrahimu Ajib kwa Yanga.

Miezi mitano baadaye katika mchezo mwingine wa watani wa jadi macho na masikio ya mashabiki wa Simba na Yanga yamehama kutoka kwa Okwi na Ajibu na sasa habari ya mjini ni Heritier Makambo na Meddie Kagere.

Msimu huu tayari inaonekana kabisa na iko wazi mechi ya watani wa jadi ipo mikononi mwa Kagere na Makambo ndiyo waliopepa presha zaidi na kuwatua mizigo Okwi na Ajib ambao wamekuwa wanasuasua mpaka hivi sasa.

Uwezo wa Kagere tangu amejiunga katika timu hiyo umemfanya aifungie timu yake mabao manne katika Ligi Kuu, huku Okwi akiwa hajaifungia timu yake bao lolote mpaka hivi sasa.

Kasi yake Kagere amekuwa mchezaji pekee anayeongelewa mara kwa mara na mashabiki wa soka kuliko mchezaji yoyote hivi sasa katika kikosi cha Simba licha ya kwamba John Bocco alifunga mabao mawili dhidi ya Mwadui lakini hata hivyo Kagere naye hakuwa nyuma kwani alifunga na kufanya watoke kifua mbele 3-1 katika mchezo huo.

Huko Yanga hivi sasa ukimuondoa Beno Kakolanya kutokana na kiwango chake alichokionyesha katika michezo kadhaa ya Ligi, basi anafuata mshambuliaji Makambo.

Makambo licha ya ugeni katika ligi, mpaka hivi sasa tayari ameshaifungia timu yake mabao mawili katika Ligi Kuu.

Upambanaji wake akiwa na mabeki wa timu pinzani umewafanya mashabiki waone kabisa kwamba aina ya mchezaji kama Donald Ngoma amesharejea katika kikosi chao.

Uwezo wa kukaa na mpira mchezaji huyu kunawafanya mashabiki wa Yanga wawe na amani muda wote.

Wakati huo huo mshambuliaji wao mwingine, Ibrahim Ajib, naye amekuja kivingine kuelekea katika pambano hili baada ya kuhusika katika magoli ya hivi karibuni.

Chanzo: mwananchi.co.tz