Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Juma Mahadhi alipopiga magoti kuomba msamaha Yanga

988 Sequence 01.Still0141 TZW

Wed, 3 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Staa wa Yanga Juma Mahadhi ambaye amewahi kuonesha uwezo na kuitwa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, hivi karibuni baadhi ya mashabiki na wapenzi wa soka waliwahi kutuhumu uwezo wa mchezaji huyo kushuka kwa uzembe ukizingatia ana umri mdogo.

Jumanne ya January 2 2018 Yanga wakielekea kuanza mchezo wao wa kwanza wa hatua ya Makundi wa Kombe la Mapinduzi Juma Mahadhi kabla ya mchezo alitumia ukurasa wake wa instagram kuomba radhi uongozi na mashabiki kwa kukiri kuwa aliteleza na anaahidi kuwa Mahadhi mpya.

Juma Mahadhi baada ya kuandika ujumbe huo wa wazi kupitia ukurasa wake wa instagram jioni ya January 2 alikuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichocheza dhidi ya Mlandege na kupata ushindi wa magoli 2-1 huku Juma Mahadhi akifunga magoli yote mawili na kuwapigia magoti mashabiki akiomba msamaha.

Huu ndio Ujumbe wa kuomba radhi wa Juma Mahadhi aliyouandika saa chache kabla ya kucheza game na kuifungia Yanga magoli mawili dakika ya 6 na 36.

“Asalam alykum ndg zangu katika Imani haja yangu kwenu ni kuomba radhi kwa mashabiki wangu wote na wapnz wote wa mpira wa miguu duniani, nakiri kufanya makosa hapo nyuma na nimejifunza mengi kupitia nyinyi nawaomba sana radhi”

“Haja ya moyo wangu ni kutataka kufikia malengo yangu niliyojiweka lakini kwa mwaka huu ilikua ngumu sana kutokana na changamoto nilizokutana nao”

Sasa ombi langu kwenu Mashabiki,Viongozi na bench la ufundi ni kuwamba kijana wenu nahitaj msamaha kama niliwakosea bado nahitaji nafasi naamin siwez kurudia kosa kwani nimejifunza mengi naahidi kuwa Mahadhi mpya”

“Naomba Imani yenu kwangu na kama mnaona bado naitajika katika timu yangu pendwa Yanga SC, tumaini langu kilio changu kimewafikia nahitaji sasa kuanza mwaka mpya nikiwa kijana mwema na mpya Asanteni sana nawapenda wote”

SportPesa imetangaza kufuta udhamini katika michezo yote Kenya

Chanzo: millardayo.com