Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Judo kumuenzi kwa kupata ushindi

E35a54a9e3b72cd942defd36a2b0dee2 Judo kumuenzi kwa kupata ushindi

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

CHAMA cha Mchezo wa Judo Tanzania (Jata) kimesema kitamuenzi Rais wa Tano, John Magufuli kwa kuhakikisha wanakwenda kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Moja ya shindano lijalo wanalotarajia kushiriki ni la Afrika la kufuzu Olimpiki litakalofanyika Morocco Mei mwaka huu, ambapo wanaishukuru Serikali ya Rais Magufuli kwasababu iliahidi kuwalipia kambi na nauli kwenda huko.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana Katibu Mkuu wa Jata Innocent Mallya alisema serikali imewalipia kambi na wanatarajia kuingia Machi 25, mwaka huu Moshi, Kilimanjaro.

“Tunashukuru serikali na tutamuenzi Rais Magufuli kwa mchango wake, nakumbuka aliwahi kusema kuwa timu zikienda nje ya nchi zihakikishe zinafanya vizuri na sisi tutajitahidi kwenda kufanya vizuri,”alisema.

Alisema kupitia mchango wa serikali yake timu ya taifa ya wachezaji wanne baada ya kukaa kambini italipiwa nauli kwenda Morocco na hilo wanajivunia kwake.

Mallya aliwataja wachezaji hao watakaoingia kambini kuwa ni Anangise Kwele, Andrew Thomas, Abdurabi Alawi, Mussa Sheki na Kocha Zaidi Hamis.

Mbali na hao, wanayokumbuka mengine ni namna huduma za afya zilivyokuwa za bei ya chini kiasi kwamba wanaweza kuwakatia wachezaji bima za afya.

Katibu huyo alisema wachezaji wengi wanaenda kutibiwa kwa bima za afya kutokana na kurahisishiwa mambo mengi ikiwemo kupata bima kwa bei nafuu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz