Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Joshua Cheptegei kutoka Uganda aibuka na Medali Olimpiki

Mwanariadha Wa Uganda,Cheptegei Mwanariadha wa Uganda, Joshua Cheptegei

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanariadha wa Uganda Joshua Cheptegei ameshinda medali yake ya pili kwenye Mashindano ya Olimpiki yanayoendelea mjini Tokyo nchni Japan, wakati aliponyakua medali ya dhahabu katika mbio za mita 5,000.

hii ni Medali ya pili kwa Mwanariadha huyo baada ya hapo awalikushinda medali ya fedha alioshinda katika mbio za mita 10,000.

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 24 alimaliza mbele ya Mzaliwa wa Somalia raia wa Canada Mohammed Ahmed, ambaye alishinda fedha, na Mmarekani mwenye asili ya Kenya Paul Chelimo, ambaye alichukua medali ya shaba.

Cheptegei anakuwa raia wa kwanza wa Uganda katika historia kushinda medali mbili za Olimpiki baada ya kushinda fedha katika mita 10,000 za wanaume wiki moja iliyopita.

Chelimo wa Marekani alijirusha utepeni kumnyima Mkenya Nicholas Kipkorir Kimemi medali ya shaba .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live