Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jose Mourinho amtumia barua nzito kikongwe mwenye miaka 94

2255 48B422AD00000578 5325091 Image A 4 1517229529976 TZW

Tue, 30 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho ametumia muda wake kumuandikia barua shabiki wa timu hiyo mzee mwenye umri wa miaka 94 badala ya kujiandaa dhidi ya Tottenham Hotspur mchezo utakao fanyika katika dimba la Wembley hapo kesho siku ya Jumatano.



Nakutakia maisha marefu shabiki, Fredrick Schofield  na uweze kupata unafuu na kupona haraka dhidi ya ugonjwa huo wa kiarusi hii imekuja baada ya kumfuatilia kwa karibu.

“Sisi sote tumemevutiwa kwa kujitolea kwako kwa muda wote Manchester United,” ameyasema hayo Mourinho ndani ya barua yake.

“Nilitaka kukuandikia neno la shukurani kwa sapoti yako na kujitolea kwako ndani ya klabu hii.”

Mourinho amesaini barua hiyo aliyomuambia Schofield  kwamba yeye mwenyewe, wachezaji na wafanyakazi wote wanamfikiria hali ambayo familia yam zee huyo ilishikwa na bumbuwazi kwa kuipata barua hiyo iliyoelekezwa kwenda kwa kikongwe huyo.





 
Chanzo: bongo5.com