Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

John Bocco na matumaini ya Taifa Stars

BOCCO 1 0 John Bocco na matumaini ya Taifa Stars

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: eatv.tv

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', John Bocco amesema ana matumaini makubwa Stars ina nafasi ya kufanya vizuri na kufuzu michuano ya kimataifa ya Afrika kwa timu za taifa 'AFCON' 2021 itakayofanyika nchini Cameroon.

Submitted by George David on Jumanne , 23rd Mar , 2021 Mshambuliaji wa Taifa Stars, John Bocco (kulia) akiwa na kiungo Himid Mao (kushoto).

Bocco amesema “Tuna nafasi ya kufuzu na kucheza mashindano haya. Itakuwa vizuri tukifuzu kwa mara ya pili mfululizo, itakuwa jambo zuri kwa kwenye mpira wa Tanzania. Utakuwa ni ujumbe mkubwa kwa wote kuwa mpira wetu umekuwa na kuongezeka ubora”.

“Ijapokuwa tunapaswa kujitoa kwa uwezo wetu wote ili tustahili kupata nafasi AFCON. Tunapaswa kuonesha njaa yetu uwanjani”.

“Maandalizi yamekuwa mazuri kwetu, tunafanya kila kitu kutokana na mipango tuliyojiwekea”.

“Kocha amekuwa anatuweka kwenye mazingira mazuri, anajaribu mbinu mbalimbali ili tufuzu. Itakuwa juu yetu wachezaqji kufuata maelekezo, kuonesha ubora wetu uwanjani na nina imani tutafuzu”.

Ikumbukwe kuwa Taifa Stars itashuka dimbani tarehe 25 Machi 2021 dhidi ya Equatorial Guinea kuwania nafasi ya kufuzu AFCON na kukipiga na Libya jijini Dar es Salaam tarehe 30 Machi 2021.

Ili Stars ifuzu inahitaji kushika nafasi ya pili ambapo itawalazimu kushinda michezo yote miwili ili ifikishe alama 10 kuungana na kinara wa kundi hilo, kundi J, timu ya Tunisia wakati hivi sasa nafasi ya pili inashikiliwa na Equatorial Guinea mwenye alama 6 na Libya akishika mkia kwa alama 6.

Chanzo: eatv.tv