Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jinamizi la penalti lamnyima usingizi Messi

9450 Pic+penat TZWeb

Mon, 18 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Lionel Messi ameeleza maumivu anayosikia baada ya kukosa mkwaju wa penalti katika mchezo dhidi ya Iceland.

Mshambuliaji huyo alikosa penalti katika mchezo ambao Argentina ilitoka sare ya bao 1-1 na Iceland katika Fainali za Kombe la Dunia.

Mkwaju huo wa penalti umeibua mjadala kila kona ya dunia hasa baada ya hasimu wake Cristiano Ronaldo kuifungia Ureno mabao matatu dhidi ya Hispania.

Mamia ya mashabiki Argentina wamepokea matokeo hayo kwa hisia tofauti wengine wakimpa lawama mshambuliaji huyo wa Barcelona na baadhi walimtetea.

Messi amekuwa katika mazingira magumu ya kuivusha Argentina katika mashindano makubwa ya kimataifa licha ya kucheza vyema katika kikosi cha Barcelona.

Mshambliaji huyo mwenye miaka 30, jana alitoa ya moyoni anavyopata uchungu, baada ya penalti yake kupanguliwa na kipa Hannes Halldorsson.

“Nina uchungu kukosa penalti. Tulikuwa na kila sababu ya kupata pointi tatu ambazo zingekuwa mwanzo mzuri kwetu. Kuanza kwa ushindi siku zote ni jambo jema, lakini tunapaswa kusahau na kujipanga kwa mchezo ujao dhidi ya Croatia,” alisema Messi.

Pia Messi alisema mchezo ulikuwa mgumu kwa kuwa wapinzani wao walicheza kwa kujilinda na kutotoa nafasi kwao kupata nafasi za kufunga.

Kauli ya mchezaji huyo bora wa dunia mara tano, imeungwa mkono na kocha Jorge Sampaoli aliyedai kuwa mbinu hiyo iliwanyima ushindi.

Wakati Messi akianza vibaya fainali hizo, Ronaldo alipachika mabao matatu ‘hat trick’ katika mchezo ambao Ureno ilishinda mabao 3-3 dhidi ya Hispania.

Wachezaji hao ambao kila mmoja ametwaa tuzo ya mchezaji bora mara tano, wanatupiwa jicho na mashabiki wengi duniani.

Messi anacheza Barcelona na Ronaldo Real Madrid ambapo kila mmoja anajiona bora zaidi ya mwingine katika medani ya soka.

Chanzo: mwananchi.co.tz