Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jezi Michael Jordan yaweka rekodi, yauzwa Bil. 23

Jezi Ya Jordan Jezi Michael Jordan yaweka rekodi, yauzwa Bil. 23

Fri, 16 Sep 2022 Chanzo: BBC

Jezi iliyovaliwa na nyota wa mpira wa vikapu Michael Jordan wakati wa mchezo wa ufunguzi wa Fainali za NBA za 1998 imeuzwa na kuweka rekodi ya kiasi cha dola milioni 10.1 (Bil. 23.3).

Hii ndio bidhaa kubwa zaidi katikakumbukumbu za michezo ambayo imeweka historia. Mnada wa Sotheby's unasema jezi hiyo iliibua "msisimko mkubwa" kutoka kwa mashabiki.

Ilikuwa kumbukumbu ya msimu wa michezo iliyorekodiwa katika makala ya Netflix The Last Dance ambayo ilishuhudia Jordan akishinda taji lake la sita na la mwisho la NBA.

Siku ya Alhamisi, Sotheby's ilisema jezi ya Jordan ya Chicago Bulls ilivutia jumla ya zabuni 20.

"Matokeo ya leo ya yaliyovunja rekodi... yanampa nguvu Michael Jordan kama G.O.A.T(Greatest Of All Time) asiyepingwa, kuthibitisha jina lake na urithi wake usio na kifani ni muhimu kama ilivyokuwa karibu miaka 25 iliyopita," Wachter alisema.

Jezi hiyo ilivuka rekodi ya awali ya $9.28m, iliyolipiwa shati iliyovaliwa na nyota wa soka Diego Maradona kwenye Kombe la Dunia la 1986.

Jordan anaonekana na wengi kama mchezaji bora katika historia ya mpira wa vikapu. Alitumia muda mwingi kuchezea Chicago Bulls, akawa nyota wa kimataifa na kusaidia kuinua ligi ya NBA kote ulimwenguni.

Jordan, ambaye sasa ana umri wa miaka 59, alitundika aliachana na mpira wa kikapu kwa mara ya mwisho mnamo 2003.

Chanzo: BBC