Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Dewji lavamia Azam

49173 Azam+pic

Thu, 28 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

MABOSI wa klabu ya Simba safari hii hawataki utani kabisa kwani, wameshaaanza kuhakikisha wanatanua kikosi chao kuelekea katika msimu ujao.

Simba wanataka kuendelea kuwa na kikosi kipana na chenye ushindani ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika mashindano yote wanayoshiriki.

Vigogo hao wameanza kutupa karata zao kimya kimya kwa wachezaji ambao, wanahitajika huku wakivamia Azam kubeba mastaa wawili wa maana.

Inafahamika kuwa, straika matata aliyetesa na Yanga, Obrey Chirwa amekuwa kwenye mazungumzo na bosi mmoja wa Msimbazi, na mpaka sasa ameshindwa kufikia makubaliano ya mkataba mpya na mabosi wa Azam FC.

Hata hivyo, Mwanaspoti linafahamu kuwa mabosi wa Simba ambayo kwa sasa iko chini ya uwekezaji wa Mfanyabiashara, Mohamed Dewji (MO), baada ya kufanikisha kwa asilimia fulani kuzuia Chirwa kuongeza mkataba Azam, wameanza kumpigia hesabu za kufa mtu beki Yakub Mohammed, anayekipiga katika kikosi cha Azam.

Vigogo hao inaelezwa kuwa walimtumia rafiki wa karibu wa beki huyo kuzungumza naye ili kuona namna anavyoweza kusaini mkataba katika kikosi chao, lakini mchezaji huyo aligoma kutokana na kusalia na mkataba na waajiri wake Azam.

Mwanaspoti limezungumza na rafiki wa karibu wa mchezaji huyo, ambapo alikiri mabosi wa Simba kumhitaji Yakub, lakini mwenyewe amekuwa akiwayumbisha.

“Kweli wamekuwa wakizungumza naye na kuhitaji kumpa mkataba, lakini amekuwa akiwazungusha kwa sababu Azam FC wamemuekea ofa mezani ya mkataba mpya,” alisema.

Mwanaspoti lilizungumza na Yakub mwenyewe kuhusiana na dili la Simba, lakini hakuweka wazi zaidi ya kusema kwa kifupi kwamba, bado ana mkataba na Azam.

Wakati huo huo Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu alisema kwamba kuhusu suala la usajili mwaliamu ndio mwenye kauli ya mwisho kuzungumzia.

“Mwalimu ndiye mwenye kauli ya mwisho ya kuzungumza kuhusu nani aingie na nani asajiliwe ni mwalimu na hata nafasi ambazo zinahitajika ni yeye pia,” alisema.

Mwanaspoti linafahamu kabisa kuwa mchezaji huyo bado ana mkataba ambao, utamuweka katika kikosi cha Azam mpaka Desemba, mwaka huu.

Yakub alijiunga na Azam Desemba 16, 2016 akitokea Aduana Stars ya Ghana, ambapo kwa sasa ametokea kuwa mchezaji tegemeo pale Azam.



Chanzo: mwananchi.co.tz