Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jembe la kazi Yanga Lawasili Kambini

7744fb671be6c3b2daa59550705d21d8?fit=1280%2C720&ssl=1 Jembe la kazi Yanga Lawasili Kambini

Thu, 25 Mar 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Jembe la kazi Yanga Lawasili Kambini March 25, 2021 by Global Publishers



DIKCSON Job, beki wa kati wa Yanga, jana Jumatano aliwasili kambini baada ya Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen kumuweka kando katika wachezaji walioenda kupambana na Equatorial Guinea.

Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa Job, zilieleza kuwa, nyota huyo baada ya kurejea Bongo akitokea Kenya ambapo Taifa Stars ilipiga kambi, kwanza alielekea kwao Morogoro, kisha akaenda kambini.

“Job amerejea Tanzania tayari kwa ajili ya majukumu ya timu yake, alipotua alienda Morogoro, kisha leo (jana Jumatano) akaingia kambini walipo wenzake kule Kigamboni,” alisema mtu huyo.

Alipotafutwa Job, alisema amerudi Tanzania kwa ajili ya kuendelea na majukumu mengine ya timu yake huku akiweka wazi maendeleo ya majeraha yake.

“Ni kweli nilipata majeraha madogo wakati wa maandalizi ya mwisho ya mchezo dhidi ya Equatorial Guinea.“Hii ni kutokana na kurejea kutoka majeruhi, hivyo sikuwa sawa, nilishauriwa kupata mapumziko kidogo, lakini kwa sasa naendelea vizuri.

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA NA JOEL THOMAS

Chanzo: globalpublishers.co.tz