Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho ameeleza kuwa anahitaji kusajili viungo wawili wakati wa dirisha la majira ya joto.
Manchester United inatarajia kumpoteza Michael Carrick ambayo anaelekea kustaafu soka na kujiunga na benchi la ufundi la timu hiyo wakati huo huo Marouane Fellaini akitimka zake Old Trafford.
Mourinho anahitaji mtu atakayeweza kuwa na Nemanja Matic na pia kumletea ushindani Paul Pogba na Juan Mata.
Hawa wafuatao huwenda wakaziba nafasi hizo mbili zinazotarajiwa kubaki wazi.
JEAN MICHAEL SERI
Klabu anayoichezea sasa ni OGC Nice
Thamani yake ni pauni milioni 35
Jean Michael Seri umri wake ni miaka 26, kiungo wa timu ya taifa ya Ivory Coast, alikosa nafasi ya kujiunga na Barcelona msimu uliyopita.
SERGEJ MILINKOVIC SAVIC
Klabu yake ya sasa ni Lazio
Thamani yake ni pauni milioni 80.
Sergeji mwenye umri wa miaka 23 anauwezo wa hali ya juu lakini pia ni rafiki wa zamani wa Nemanja Matic katika timu ya taifa ya Serbia.
JORGINHO
Timu yake ya sasa ni Napoli
Thamani yake ni pauni milioni 35
Jorginho mwenye umri wa miaka 26 amekuwa mchezaji muhimu ndani ya Napoli .
TONI KROOS
Timu yake ya sasa Real Madrid
Thamani yake ni pauni milioni 30
Toni anaweza kuziba nafasi ya Carrick bilashaka kutokana na kiwango kikubwa alicho nacho.
VICTOR WANYAMA
Anakipiga katika timu ya Tottenham
Thamani yake ni pauni milioni 40
United na Liverpool wamekuwa wakivutiwa kwa mchezaji huyu wakimataifa wa Kenya ambaye amerejea kutoka katika majeraha.
Klabu zote zinavutiwa na kiwango cha mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 26 anayecheza timu ya Tottenham.
WILLIAN
Anacheza timu ya Chelsea
Thamani yake ni pauni milioni 40
Jose Mourinho amesema haitaji mshambuliaji katika dirisha la usajili wa majira ya joto ili huvutiwa na kiwango cha Willian hasa katika umaliziaji.