Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Je ni kweli Simba inakamiwa na timu pinzani?

76930449 Je ni kweli Simba inakamiwa na timu pinzani?

Thu, 4 Nov 2021 Chanzo: eatv.tv

Patashika ya Ligi Kuu Tanzania bara imeendelea kushika kasi yake lakini matukio kadhaa yamekuwa yakijitokeza Viwanjani huku kadi nyekundu zikiendelea kuonyeshwa kwa wachezaji katika vilabu mbalimbali.

Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Hitimana Thiery akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mchezo.

Jumla ya wachezaji wanne wa timu pinzani wameonyeshwa kadi nyekundu dhidi ya Simba SC kwenye michezo ya Ligi kuu Tanzania bara tangu kuanza kwa msimu wa 2021/2022.

Idadi hiyo imetimia baada ya hapo jana kiungo wa Namungo FC Abdul azizz Makame kupata kadi nyekundi baada ya kumchezea madhambi mlinzi wa kulia wa Simba Shomari Kapombe.

Wachezaji wengine waliopata kadi nyekundu ni Benedict Jocob wa Coastal Union, juma Kakuti wa Polisi Tanzania, na Anuary Jabir wa Polisi Tanzania.

Na mchezo wa hapo jana Simba ilishinda bao 1-0 lililofungwa na Meddie Kagere na kuifanya Simba kufikisha alama 11 na wamepanda mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi wakiwa na alama 11 ikiwa ni 4 nyuma na vinara Yanga wenye alama 15.

Chanzo: eatv.tv