Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

James Harden mkali muda wote NBA?

HARDEEEEN James Harden mkali muda wote NBA?

Wed, 1 Dec 2021 Chanzo: eatv.tv

Nyota wa Brooklyn Nets, James Harden ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wanne kwenye Historia ya NBA kuvuna alama nyingi za 3-pointers kwenye regular season kwa kufikisha alama 2, 500.

Harden amefikia alama hizo baada ya alfajiri ya kuamkia leo Disemba 1, 2021  kufunga alama 24 zilizotokana na 3-pointers 8 hivyo kufikisha jumla ya alama 34, rebound 10 na Assist 8 na kuisaidia Brooklyn kushinda 112-110 New York Nicks.

Baada ya kufikisha alama 2, 500 za 3-poimters, Harden sasa ni wanne kwenye histroia ya NBA nyuma ya Reggie Miller (2,560), Stephen Curry (2,937) na kinara Rey Allen (2,973).

Lakini kwa wachezaji ambao wanaendelea kucheza mpaka hivi sasa, Harden ni mchezaji wa pili nyuma ya Stephen Curry (2,937) wa Golden State Warriors mwenye umri wa miaka 33.

 

 

Chanzo: eatv.tv