Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JPM ameleta nidhamu ya fedha michezoni

834425165dbff5418541fc365cfe8ae3.png JPM ameleta nidhamu ya fedha michezoni

Sat, 20 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MIONGONI mwa mambo ambayo yataendelea kukumbukwa na wanamichezo yaliyofanyika katika kipindi cha rais John Magufuli ni kitendo cha kuleta nidhamu ya matumizi mazuri ya ofi si.

Sehemu ambayo ilikuwa haiangaliwi sana ilikuwa ni katika michezo hasa soka ambako kulijaa madudu mengi lakini umakini na ufuatiliaji wake uliibua mengi ikiwamo sakata la utakatishaji wa fedha kutoka Shirikisho la soka la kimataifa, FIFA na kuhalalisha malipo kinyume cha utaratibu.

Rejea kesi ambazo ziliibuliwa katika Shirikisho la soka nchini TFF, kuhusu matumizi mabaya ya ofisi ambapo rais Jamali Malinzi na katibu mkuu wake Celestine Mwesigwa na mhasibu Nsiande Isawafo Mwanga walituhumiwa.

Malinzi, Mwesigwa na Nsiande walikuwa na kesi ya utakatishaji wa fedha Dola za Marekani 375, 418 (zaidi ya Sh milioni 840) wakati wakijua fedha hizo ni matokeo ya mapato ya kughushi.

Wakati hayo yakiwakuta TFF, hali kama hiyo iliwakuta pia baadhi ya viongozi wa klabu ya Simba, akiwamo rais wa klabu hiyo Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange 'Kaburu' ambao walishitakiwa kwa makosa ya utakatishaji fedha.

Kwa pamoja washtakiwa hao wanadaiwa kuwa walikula njama ya kughushi fomu ya maombi ya kuhamisha fedha ya Machi 15,2016 wakionesha Klabu ya Simba inalipa mkopo wa Dola za Marekani 300,000 kwa Evans Aveva wakati si kweli.

Lakini pia wengine walioingia katika kesi hiyo ni pamoja na Franklin Lauwo na Zacharia Hanspope, kipindi cha Magufuli hakukuwa na masikhara hasa katika upande wa fedha.

Katika kipindi chake tulishuhudia aliyekuwa makamu wa rais wa TFF, Michael Wambura akifungiwa maisha kujihusisha na mchezo wa soka.

Wambura alikuwa na makosa ya matatu ambayo ni Kupokea/kuchukua fedha za TFF za malipo ambayo hayakuwa halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(1) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013.

Kughushi barua ya kuelekeza alipwe malipo ya kampuni ya JEKC SYSTEMS LIMITED huku akijua malipo hayo sio halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013.

Kufanya vitendo vinavyoshusha Hadhi ya Shirikisho ikiwa ni kinyume na ibara ya 50(1) ya Katiba ya TFF (kama ilivyorekebishwa 2015) Hukumu hiyo ilitolewa (Januari 22, 2019) na kutumwa TFF.

Kamati ya nidhamu ya FIFA chini ya mwenyekiti wake Anin Yeboah wa Ghana, ilikazia hukumu ya kamati ya rufani ya maadili ya TFF iliyotolewa Aprili 6, 2018, hivyo kutokana na kamati ya nidhamu ya FIFA kukazia hukumu ya kamati ya rufani ya maadili ya TFF,Wambura hatakiwi kujihusisha na masuala ya mpira wa miguu duniani kote.

Sakata hilo lilimfikisha Wambura mahakamani, baadae akanusurika na hukumu baada ya Magufuli kuagiza wote walio na kesi ya ubadhirifu kurudisha fedha hizo na kuachiwa huru ndipo kiongozi huyo machachari wa soka akanusurika.

Uamuzi huo wa Magufuli pia ulimnusuru Malinzi na Mwesigwa walioachiwa huru baada ya kukidhi masharti hayo baada ya kusota rumande muda mrefu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz