Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JKT Tanzania yaikimbiza Yanga

JKT+RUVU+KIKOSI 752125 0 JKT Tanzania yaikimbiza Yanga

Thu, 2 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KOCHA Mkuu wa JKT Tanzania, Mohammed Abdallah 'Bares' amesema lengo namba moja la timu yake ni kuhakikisha wanamaliza msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/20 wakiwa katika nafasi tano za juu.

Kwa sasa JKT Tanzania yenye pointi 47, ipo katika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi hiyo baada ya kucheza mechi 32.

Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Bares alisema kikosi chake kipo tayari kwa ushindani na anaamini wachezaji wake watapambana kupata matokeo mazuri katika mechi zake zilizobaki.

Bares alisema kuna ushindani mkubwa katika ligi hasa kipindi hiki cha lala salama kwa kila timu kuhitaji pointi ili kujiokoa na janga la kushuka daraja.

"Ushindani ni mkubwa, hilo lipo wazi ila chochote kinaweza kutokea katika ligi, hatujakata tamaa, bado tunapambana ili kuona namna gani tunafika malengo yetu," alisema Bares.

Kocha huyo alisema mikakati yake ni kupata matokeo mazuri katika mechi mbili za ugenini dhidi ya Namungo FC ambayo watacheza kwenye Uwanja wa Majaliwa Julai 4 na 8, mwaka huu watawafuata Ndanda FC kwenye dimba la Nangwanda Sijaona, Mtwara.

"Kikosi changu kipo vizuri hakuna majeruhi, tutamkosa Mwinyi Kazimoto katika mchezo dhidi ya Namungo kwa kutumikia adhabu ya kadi nyekundu, atarejea tena katika kampeni yetu tutakokwenda Mtwara kuivaa Ndanda," alisema Bares.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live