Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JKT Tanzania waigomea Bodi ya Ligi

28758 Pic+jkt TanzaniaWeb

Mon, 26 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) limetangaza mabadiliko ya mechi ya kiporo kati ya JKT Tanzania na Yanga iliyokuwa ichezwe Alhamisi ijayo jijini Tanga.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa TPLB, Boniface Wambura alisema badiliko hilo ni la kawaida na mchezo hautachezwa Mkwakwani

Hata hivyo, Katibu Mkuu JKT Tanzania, Abdul Nyumba alisema hawakubaliani na uamuzi huo kwani wamefanya maandalizi yote na wao ndio wenye haki kama wenyeji, lakini wameshangaa na kuambiwa sasa watacheza Dar na sio Tanga tena.

“Uwanja wetu wa nyumbani kwa Simba na Yanga ni Mkwakwani, Tanga. Simba tumeshacheza nao Tanga na kutufunga, mechi ijayo ilikuwa dhidi ya Yanga, kwani tumepangwa kuwa wenyeji katika mchezo huo, lakini sasa tunashangaa Bodi ya Ligi kutulazimisha tucheze Dar es Salaam na kuwapa Yanga uenyeji hii sio haki kabisa,” alisema.



Chanzo: mwananchi.co.tz