Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JKT, Magereza yaanza vyema BAMATA

BAMATA.jpeg JKT, Magereza yaanza vyema BAMATA

Sun, 12 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Timu za Kanda ya JKT na Magereza zaanza vizuri mashindano ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMATA) kwa kufanya vizuri katika michezo ya soka, wavu na netiboli.

Michezo hiyo inayofanyika Mtwara na kuhudhuriwa na wanamichezo kutoka majeshi yote nchini inaendelea kuchezwa katika viwanja mbalimbali mkoani hapa.

Ofisa Habari wa BAMATA, Kapteni Frank Malema amesema hadi sasa JKT na Magereza zinaonyesha kufanya vizuri zaidi kwa kupata ushindi kwenye mechi zao.

“Hata ukiangalia wanamichezo wanaotoka JKT na Magereza utaona tofauti ya umri na wanavipaji vingi japo magereza walipoteza mchezo mmoja wa basketball hali ya mvua lakini michezo inaendelea vizuri,” amesema Kaptain Malema na kuongeza;

“Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha uwanja unaotumika kwa mchezo wa riaza unaharibiwa na mvua tunaangalia namna ya kuuhamisha mchezo huu ili uweze kuchezewa katika uwanja wa Nangwanda sijaona.”

Kocha Kanda ya JKT, Hafidhi Tindwa amesema kuwa mashindano hayo ni mazuri lakini magumu kwakuwa yanaushindani mkubwa tofauti na miaka mingine.

“Mechi zote ni ngumu kila mmoja anatetea kanda yake haya mashindano ushindani ni mkubwa zaidi na inahamasisha na inapendeza watu wamejiandaa.”

Nahodha wa Kanda ya JKT Koplo Joyce Kaila amesema ushindani ni mkubwa mpaka sasa ushindi waliopata unawapa haasa ya kucheza zaidi ilikuttetea ubingwa.

“Matokeo yanatupa hamasa ya kuendelea kushinda ili kutetea ubingwa wetu matokeo ni mzuri tutashinda mechi zote zilizobakia ili kuendelea kuwa na ubingwa wetu.”

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amesema ameburudika na michezo hiyo huku akiwahimisha wananchi kujitokeza kuangalia michezo kama sehemu ya burudani.

“Najisikia fahari na furaha michezo hii kufanyika katika mkoa huu kwa kuwa kuna mwingiliano wa wanajeshi na wananchi pamoja na kufunguka kwa biashara mbalimbali. Mwitikio ni mkubwa zaidi lakini wananchi wanaweza kujitokeza ili kufanyabishara malimali wanajeshi ni kazi wakimaliza kazi wanakuwa wannchi hii michezo ni mizuri,” amesema Kanali Abbas.

Chanzo: Mwanaspoti