Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JK, Manji wafunika mkutano mkuu Yanga

Manji 1pic Data JK, Manji wafunika mkutano mkuu Yanga

Mon, 28 Jun 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete (JK) na Yusuf Manji ndio viongozi walioshangiliwa zaidi na wanachama kwenye mkutano mkuu wa Yanga unaoendelea jijini Dar es Salaam.

Shangwe la mashabiki hao wakati mfadhili na mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo Manji alipoingia ukumbini na wakati Rais mstaafu, Kikwete akiingia lilikuwa mara dufu kulinganisha na walivyowapokea viongozi wengine.

Manji aliingia ukumbini saa 4:58 asubuhi akiwa amezungukwa na makomandoo wa Yanga, kuingia kwake kulisimamisha shughuli ukumbini kwa muda kama ambavyo Rais mstaafu, Kikwete alipoingia ukumbini saa 6:10 na kushangiliwa na wanachama wote ukumbini hapo.

Baada ya Rais mstaafu Kikwete kuingia, wanachama wa Yanga walifungua mkutano kwa sala na duwa kwa dakika 13.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz