Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JANUAR MAKAMBA AMJIBU MOO DEWJI ISHU YA USAJILI.

Mo J?fit=800%2C445 JANUAR MAKAMBA AMJIBU MOO DEWJI ISHU YA USAJILI.

Wed, 5 Aug 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Baada ya Tweet ya Jana ya Tajiri wa Mabingwa wa Soka Tanzania, moodewji aliyosema “Timu nzuri hazihitaji kusajili sana”, neno lake hilo limepokelewa kwa hisia tofauti na Mnazi kindakindaki wa Simba SC , Mh. January Makamba.

Kutokea Twitter, Mh January Makamba ameonekana akiwa na maoni tofauti, Yeye anasema “Tuna timu nzuri lakini kwa lengo letu la kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika, tunahitaji nafasi tatu za wachezaji wa kiwango cha kucheza Ligi ya mabingwa. Kwanza tunahitaji, Beki kijana mwenye spidi na uwezo wa kucheza ‘Set-Pieces’ (Mipira ya kona), Pili tunahitaji Beki wa kulia mwenye discipline ya ukabaji, na Mfungaji Kijana, mwenye speed, njaa ya goli na mwenye uwezo mzuri wa kuwapiga vyenga mabeki”.

Sio hvyo tu, akaongeza kuwa ”Tafadhali naomba mumpe Shiboub nafasi zaidi kwenye timu kama Mido wa kati”

Story by www.dimbani.co.tz

Chanzo: zanzibar24.co.tz