Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Infantino na Kombe la Dunia kila miaka miwili

Fifa Infantino na Kombe la Dunia kila miaka miwili

Wed, 20 Oct 2021 Chanzo: ippmedia.com

RAIS wa Shirikisho la Soka duniani (FIFA), Gianni Infantino, ameelezea umuhimu wa Kombe la Dunia la wanaume na wanawake kufanyika kila baada ya miaka miwili.

Infantino amebainisha kwamba kumekuwa na ushirikishwa wa maoni kwa ndani ya chombo hicho na kwa pande zote zinazohusika kuhusu mpango huo na amesisitiza kuna faida nyingi zaidi chanya zitakazokuja kwa michuano hiyo kufanyika mara kwa mara.

"Tunachambua kama inawezekana kuandaa michuano ya Kombe la Dunia kila baada ya miaka miwili, kama itakuwa na faida chanya kwa soka letu," alisema Infantino Jumatatu akiwa kwenye Mji Mkuu wa Argentina, Buenos Aires.

"Kuna wazo hilo na sasa linafanyiwa kazi ndani na kutafuta ushauri kutoka pande zote. Kuna baadhi wanaunga mkono na wengine hawakubaliani na wazo hili."

Mpango wa Kombe la Dunia kufanyika kila baada ya miaka miwili unaoungwa mkono na Infantino, unapingwa vikali na Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA), Shirikisho la Soka la Amerika Kusini (CONMEBOL), Chama cha Klabu za Ulaya chenye timu 234, pamoja na Chama cha Wachezaji wa Kulipwa duniani (FIFPRO).

"Faida ya kuandaa michuano ya Kombe la Dunia kila baada ya miaka miwili inaonekana wazi kabisa kwa upande wangu," alisema Infantino.

Bara la Ulaya limeandaa michuano ya Kombe la Dunia mara 11, mara mbili zaidi kuliko bara lingine lolote.

Amerika Kusini limeandaa michuano hiyo mara tano, huku Afrika na Asia zikiandaa mara moja, na mwaka 2022 michuano hiyo itafanyika nchini Qatar.

Chanzo: ippmedia.com