Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ilfya aitamani Simba Tena

ILANFYA Charles Ilnfya, kiungo Azam FC

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji Charles Ilnfya ambaye alipelekwa kwa mkopo ndani ya KMC ili akuze kiwango chake, amesema kuwa kwa sasa yupo tayari kurudi Simba ili kuendelea pale alipoishia.

Ilanfya alisema kuwa kwa sasa anafikiria kurudi Simba kwa kuwa uwezo anao na anatambua kwamba uwezo wake ni mkubwa.

“Nilipokuwa ndani ya KMC nilikuwa ninawasiliana na viongozi kutoka Simba ambapo walikuwa wananifuatilia pia jambo ambalo lilifanya niongeze juhudi.

“Kwa hapa ambapo nipo ninaweza kusema kwamba uwezo wa kucheza Simba upo na ninaweza hivyo ni suala la kusubiri na kuona mambo yatakuaje,”

Nyota huyo alipewa dili la miaka miwili ndani ya Simba, alikwama kufurukuta zama za Sven Vandenbroeck na alitolewa kwa mkopo kurudi kwenye timu yake ya zamani KMC ambapo huko aliweza kutupia mabao sita na pasi mbili za mabao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live