Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ile baki tu baki inarudi, Manji apagawisha mastaa Yanga

Yangaa Pic Data Ile baki tu baki inarudi, Manji apagawisha mastaa Yanga

Wed, 23 Jun 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KITENDO cha Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kulipia kadi yake ya uanachama juzi Ijumaa kimeibua mzuka wa mabeki wawili mahiri wa zamani wa timu hiyo ambao wamesisitiza kwamba; “Karudi? ile baki tu baki inarudi.”

Wakimaanisha kwamba ile rekodi ya Yanga kubeba makombe misimu mfululizo kama ilivyokuwa enzi za Manji akiwa Mwenyekiti zinarudi.

Mwanaspoti jana liliripoti habari ya Manji kulipia kadi yake ya uanachama juzi Ijumaa tayari kwa mkutano mkuu wa wanachama Jumapili ijayo Jijini Dar es Salaam.

Beki mwili nyumba,Samson Mwamanda alisema kitendo cha Manji kuilipia kadi yake ya uanachama kimewafurahisha Wanayanga na kinaashiria neema inakuja ya kuchukua mataji kama ilivyokuwa kipindi cha uongozi wake.

“Japokuwa kulipia kadi ni haki ya kila mwanachama wa Yanga, ila naamini anaweza akafanya kitu cha kuunganisha nguvu na GSM na tukawa na kikosi chenye ushindani wa kuchukua mataji baki tu baki kama alivyofanya wakati akiwa mwenyekiti wetu,” alisema staa huyo wa zamani wa Prisons.

Mlinzi mwingine wa zamani wa Yanga, John Mwansasu alisema ; “Ukitaka kufika haraka nenda mwenyewe, ukitaka kufika mbali unganisha nguvu na wengine, maana yangu ni kwamba hata kama Manji atarejea tena kuisapoti Yanga ili waifikishe mbali wanatakiwa kuunganisha nguvu na GSM na kuweka mikakati imara na kuondoa janjajanja zilizopo ambazo zinapunguza thamani ya klabu.

Aliongeza kuwa; “Leo hii ligi yetu inaonekana ni miongoni mwa ligi bora Afrika ni kwasababu ya Simba kulingana na uwekezaji waliouweka na kuamua kuweka pembeni janjajanja, hicho ndicho kinachotakiwa kufanyika Yanga, kuwa na viongozi wenye malengo ambao wanaweza wakazitumia vyema rasimali zilizopo.” Alisema kinachotakiwa Yanga kwasasa nikuondoa mazoea ya kufanya kazi na kutambua soka la kisasa linahitaji kujitoa na kwamba Manji akiunga nguvu itakuwa Yanga tishio ndani na nje ya nchi.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz