Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ihefu U20 yashindwa kupindua meza kwa Mtibwa

Mtibwa U20 Data Ihefu U20 yashindwa kupindua meza kwa Mtibwa

Sun, 2 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Timu ya vijana chini ya miaka 20 ya Mtibwa Suagr imeendeleza ubabe kwa vijana wenzao wa Ihefu Fc baada ya kuitandika bao 3-0 katika mchezo mkali uliopigwa kwenye dimba la Jamhuri Morogoro.

Katika kundi hilo, vijana wa Tanzania Prison wenyewe walikubali kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Simba katika mchezo uliofanyika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam huku Ihefu ikiwa ni mchezo wa pili ambapo katika mchezo wa kwanza walikubali kipigo bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Mbarali mkoani Mbeya.

Simba inaongoza kundi hilo C wakiwa na alama 13 sawa na mabingwa watetezi wa michuano hiyo Mtibwa Sugar kwa mabao machache ya kufunga.

Jabiri Masumbuko (wa tatu kutoka kulia) akishangilia bao la tatu dhidi ya Ihefu wakati wa michauno ya vijana chini ya umri wa miaka 20 mchezo uliofanyika uwanja wa jamhuri Morogoro na Ihefu kukubali kipigo cha bao 3-0. Picha na Juma Mtanda.

Walinzi wa Ihefu ilishindwa kuwadhibiti washambuliaji wa Mtibwa na kumruhusu, Baraka Kiumbe kufunga bao la kuongoza dakika ya 32 akiunganisha vyema mpira wa adhabu uliopigwa na Jabiri Masumbuko huku dakika 45 Saidi Kazi akifunga bao la pili.

Mtibwa ilipata bao la tatu na ushindi dakika ya 79 kwa Jabiri Masumbuko kufunga bao huku safu ya ushambuliaji ya Ihefu ikishindwa kuipatia timu yao mabao kwa nafasi walizopata na kufanya mchezo huo umalizike kwa Ihefu kukubali kipigo cha bao 3-0.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz