Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ibra Class Bigwa WBF

C2db08cb1aee149c1d5f63a234eaa41c Ibra Class Bigwa WBF

Wed, 3 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

BONDIA Ibrahim Class ameshinda mkanda wa kimataifa wa WBF baada ya kumchapa Denis Mwale kutoka Malawi kwa majaji wote watatu katika pambano la raundi 12.

Katika pambano hilo gumu lililopigwa Dar es Salaam juzi usiku, Class alionesha ubora wa hali ya juu kwenye mizunguko tofauti na kumzidi kete mpinzani wake.

Akizungumza baada ya ushindi huo Class alisema Mwale ni bondia mzuri na mgumu mwenye akili ila alijua udhaifu wake ni pumzi na yeye akatumia nafasi hiyo kumshinda.

“Mabondia ninaokutana nao safari hii wananipa changamoto kwasababu ni wagumu hawapigiki kirahisi, nilimchunguza Mwale nikagundua anakata pumzi nami nikatumia mwanya huo kumpiga,”alisema.

Alisema anashukuru kukutana na mabondia wagumu kwasababu anaamini hata akienda nje ya nchi kupambana hatakutana na wepesi na itampa nafasi ya kushinda kwa kuwa atakuwa amewazoea.

Class alisema mashabiki zake wamekuwa wanatamani ashinde kwa ‘Technical Knockout’ lakini ni vigumu kutokana na aina ya wapinzani anaokutana nao.

Kwa upande wa Mwale alisema hawezi kumlaumu mtu kwa kupoteza anafurahi amekutana na bondia mzuri na amejifunza kutokana na makosa.

“Mpinzani wangu ni bondia mgumu nina uhakika tulipambana vizuri ila mwenzangu ametumia vizuri mazingira ya nyumbani kushinda, sina wa kumlaumu nimejifunza mengi,”alisema.

Mbali na hao, wengine waliocheza katika mapambano ya utangulizi ni bondia kutoka Bagamoyo aliyepoteza mbele ya Mwanajeshi Hafidh David kwa knockout raundi ya kwanza.

Pia, Said Mlosi alivyokumbana na kichapo kutoka kwa Hashim Kilanga katika pambano la raundi nne.

Ni zamu ya Tervel Pulev kutoka Bulgaria dhidi ya Vikapita Merero kutoka Namibia. Mbulgaria Tervel Pulev amemtwanga kwa TKO Mnamibia Vikapita Merero raundi ya tisa, katika pambano la raundi 10.

Mtanzania mwingine Imani Kawaya alipihwa na Mkongo Ardi Ndemb na Happy Daud alipigwa kwa Knockout raundi ya kwanza na Mzambia Lolita Muzeya.

Chanzo: habarileo.co.tz