Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

IPC yazifungia Urusi na Belarus Olympic 2022

Urusi Baadhi wa washiriki kutoka Urusi waliozuiliwa kushiriki michezo ya Paralympic 2022

Thu, 3 Mar 2022 Chanzo: eatv.tv

Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki ya Walemavu (IPS) imezipiga marufuku nchi za Urusi na Belarus kushiriki kwenye michezo ya majira ya baridi ya Olimpiki ya Walemavu 2022 yanayotarajiwa kufunguliwa siku ya ijumaa March 4 na kumalizika mnamo March 13 mjini Beijing nchini China.

Rais wa IPC Andrew Parsons amesema kumekuwa na wito mkubwa kwa washiriki kutaka kugomea kushindana na wanamichezo kutokea nchi za Urusi na Belarus kuonesha kuchukizwa na uvamizi wa nchi ya Urusi kwa taifa la Ukraine.

"sisi wote ni waumini wa michezo kutokuchanganywa na mambo ya kisiasa lakini hili sio tatizo letu bali ni vita imesababisha na mataifa mbalimbali yamekuwa wadau wakubwa kwenye mashindano yetu na wanamichezo kutoka nchi za Urusi na Belarus ni waathirika kutokana na vitendo vya serikali yao "amesema Parsons

Wanamichezo 71 kutoka Urusi sambamba na wanamichezo 12 kutoka Belarus walipaswa kushiriki kwenye michezo hiyo huku kiongozi wa kamati ya watu wenye ulemavu ya Olympic kutoka Ukraine Valeriy Sushkevych amesema ushiriki wa nchi hiyo kwenye michezo ya majira ya baridi ya Beijing 2022 ni kiashiria kwamba nchi hiyo bado ipo hai.

Chanzo: eatv.tv