Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huko RT bado hakueleweki

69487 Riadha+picha

Fri, 2 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

MASHINDANO ya Taifa ya mchezo wa Riadha yaliyokuwa yafanyike mwishoni mwa mwezi uliopita, yameendelea kuwa kizungumkuti hadi sasa huku uongozi wa Shirikisho la Riadha Nchini (RT) likizidi kutoa sababu za kujitetea.

Katibu Mkuu wa RT, Wilhelm Gidabuday alisema, moja ya vitu vinavyochangia kushindwa kufanyika kwa mashindano hayo kwa muda sahihi ni kutopata fedha za kuendeshea.

"Tayari mdhamini ambaye ni Mamlaka ya Ngorongoro aliahidi kutoa Sh 40, lakini hadi sasa hakueleweki na ndio sababu inayochangia tushindwe kufanya kazi yetu kama kalenda ya RT inavyoonesha," alisema Gidabuday.

Aliongeza pamoja na hayo kuna madai ya wanariadha sh 6,000,000 kwa RT kitu kinachozidi kuleta ukakasi wa kuwapeleka wanariadha hao kwenye mashindano wakati wanadai stahiki zao tena kwa uongozi unaowasimamia.

Mashindano ya taifa ya riadha yanafanyika kila mwaka ikiwa ni moja ya maagizo ya Shirikisho la Riadha la Kimataifa (IAAF) kwa wanachama wake ambao hupokea ruzuku ya kuendesha shughuli zao ikiwemo mashindano ya ndani.

Chanzo: mwananchi.co.tz