Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hofu yatanda Man City kung’olea Ulaya

30225 Pic+city TanzaniaWeb

Wed, 5 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Manchester, England. Hofu imetanda baada ya kuelezwa klabu ya Manchester City inaweza kuneguliwa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Kocha Pep Guardiola, ambaye ameiwezesha timu hiyo kujihakikishia tiketi ya hatua ya 16 bora alisema litakuwa pigo la aina yake kwao, iwapo wataenguliwa katika michuano hiyo.

Gazeti la Der Spiegel la Ujerumani limesema kuwa uchunguzi mkali unaendelea ukimuhusisha bosi wa Shirikisho la soka la Kimataifa (Fifa) Gianni Infantino kwamba aliisaidia Man City kukiuka kanuni za muongozi wa matumizi ya fedha za usajili (FFP).

Ilifichuliwa kuwa Infantino alitumia kofia yake ya Rais wa Shirikisho la soka Ulaya (Uefa) kuilinda Man City isiadhibiwe wakati ikichunguzwa kwa kukiuka kanuni za FFP.

Gazeti hilo limedai kuwa mmiliki wa klabu hiyo Sheikh Mansour, alifanya udanganyifu kwa kumtumia mgongo wa mdhamini wa klabu hiyo kuficha ukweli na kukwepa kuadhibiwa Uefa.

Hata hivyo tayari Uefa imefungua uchunguzi mpya dhidi ya bilionea huyo na klabu yake kwa ujumla unaotarajiwa kuanika hadharani hivi karibuni.



Chanzo: mwananchi.co.tz